Wasafi
Nawaza kwa nini sikumjuaga zamani
Oh mama
Pendo lake zito mpaka lavunja mizani
Oh mama
Yeye na mimi kachoo nisharuka nyie
Oh mama
Wasiojua mapenzi pole jamani
Vinjali kuwa bachelor, aibu gani
Aliyeumba dunia
Akayaumba na mapenzi
Wala hakukosea
Ila mwezenu mi siwezi
Nilishapenda ila nikatendwa
Moyoni vidonda maskini roho
Mbona nilikonda licha ya kuhonga
Kuweka vibanda nishaomba poo
Mwenzangu bado hujajua, baki unicheke
Kwako yamechanua, ngoja yanyauke
Andazi si kitumbua acha mapepe
Ukipendwa tanua, kwa nini usideke?
Jama nimependa mie, nimependa mie
Nimependa mie nataka nimweke ndani
Mwenzako, nimetendwa mie, nimetendwa mie
Nimetendwa mie, mapenzi sitamani
Ana mapenzi ya bara kayachanganya na pwani
Vipi nitajinasua
Rangi kama chotara shape sio mjapani
Ana shingo si vibuaa
Ameumbika sina budi nisifie
Akipika natamani nilipie
Sehemu ya upanga uliweka kiwembe
Ndo maana mwasi, akaona ajichekee
Kwa wenzako sikia, sikia mwana
Ila kwako utalia, utalia sana
Mi likuwaga fundi, fundi zaidi yako
Power ka mirundi, ikiganda kama sumako
Nakutia pesa madegeree, asiniachee
Nikamchanganya akolee, asiwakee
Penzi upepo wa bahari, mara kusi shwari
Yakichange hatari, usiombee
Jama nimependa mie, nimependa mie
Nimependa mie nataka nimweke ndani
Mwenzako, nimetendwa mie, nimetendwa mie
Nimetendwa mie, mapenzi sitamani
Nimetendwa, aah
Mwenzako nimetendwa
Nimetendwa
Nimependa mie
Nimependa mie
Nimependa mie
Nimependa mie
Nimetendwa mie
Nimetendwa mie
Nimetendwa mie
Nimetendwa mie
Wasafi Records
Mais de 15 cursos com aulas exclusivas, materiais didáticos e exercícios por R$49,90/mês.
Tenha acesso a benefícios exclusivos no App e no Site
Chega de anúncios
Mais recursos no app do Afinador
Atendimento Prioritário
Aumente seu limite de lista
Ajude a produzir mais conteúdo