(Fraga got the recipe)
Waliniita kimbaumbau, kiguu na njia
Ila nikadharau, nikapuuzia
Leo kwao kafa nyau, yanawanukia
Kwetu twafinya pilau, yametimia
Ooh wanjara, walete bunyero ooh
Mi nataka kulimwaga razi (na makagheroo)
Waite na mapaparazi (wapate kero)
Wale wenye magho ya nazi (bando la jero)
Wapate vya kuperuzzi
Habari ziende kwa ma ex
Penzi waliodhulumu
Tena nimepata tetesi
Mmoja ataka kunywa sumu
Kisaa jamani kisaa
Nikauliza kisaa, kisa leo naolewa
Naolewa, naolewa mie (ooh sheba)
Naolewa, naolewa mie
Nilikosaga na dira kwa maneno ya waja
Ooh subira aah, mbele inafaraja
Asa chereko, ngoma lipo uwanjanii
Mwali na mideko, kama nimetoka ngomani
Aii yuko wapi mamie mwali
Aje anibebe mgongoni
Amuite daddy mwali waje
Wayarudi ya msondondo
Bibi anacheka, zawadi kaleta
Na kitenge na mkeka
Na kibunda cha pesa
(Aah aah aah)
Habari ziende kwa ma ex
Penzi waliodhulumu
Tena nimepata tetesi
Mmoja ataka kunywa sumu
Kisaa jamani kisaa
Nikauliza kisaa, kisa leo naolewa
Naolewa, naolewa mie (ooh sheba)
Naolewa, naolewa mie
Sina sina makosa (mtoto wa mwenzio)
Sina sina makosa (utajiua)
Sina sina makosa (mtoto wa mwenzio)
Sina sina makosa (utajiua buree)
Buree, buree
Mais de 15 cursos com aulas exclusivas, materiais didáticos e exercícios por R$49,90/mês.
Tenha acesso a benefícios exclusivos no App e no Site
Chega de anúncios
Mais recursos no app do Afinador
Atendimento Prioritário
Aumente seu limite de lista
Ajude a produzir mais conteúdo