Tunapojituma
Kuyaharibu makaazi yetu
Tunajihatarisha
Bila shaka twajiangamiza
Muda wetu wayoyoma
Kadri unavyosonga
Tunajiteketeza
Misitu ikiisha utavutaje mvua
Jukumu letu kuelewa
Kuwa jua, mwezi, mvua na ardhi
Wanyama pori na adinasi
Mito, milima, misitu na nyasi
Vidudu na ndege wa angani
Vimefumwa kwa pamoja
Ulimwengu ukizunguka
Kile tunachopanda
Bila shaka ndicho tutavuna
Kama jua likitua
Yale tunayofanya
Bila shaka yatatufuata
Binadamu ni tishio kubwa kwa dunia
Na vitendo anavyo fanya
Hufanya viumbe kuumia
Sasa chukua hatua
Wakati ndio sasa
Kuyahifadhi mazingira
Kupata amani
Twahitaji uwiano
Kuilinda dunia
Kwa vizazi vijavyo
Ulimwengu ukizunguka
Kile tunachopanda
Bila shaka ndicho tutavuna
Kama jua likitua
Yale tunayofanya
Bila shaka yatatufuata
Tenha acesso a benefícios exclusivos no App e no Site
Chega de anúncios
Badges exclusivas
Mais recursos no app do Afinador
Atendimento Prioritário
Aumente seu limite de lista
Ajude a produzir mais conteúdo